TETESI za usajili zinasema Manchester City imetuma ofa kumsajili kiungo wa Hispania Dani Olmo, 26, anayekipiga katika klabu ya RB Leipzig ya Ujerumani. (Foot Mercato – in French)
Olmo alikuwa na kiwango bora wakati wa michuano ya Kombe Ulaya(EURO2024) iliyomalizika Julai 14 nchini Ujerumani ambapo alishinda sehemu ya tuzo ya kiatu cha dhahabu na alitoa mchango muhimu kwa timu ya taifa ya Hispania-La Roja- iliyoweka rekodi ya kushinda taji la nne la Ulaya.
Barcelona pia inamfukuzia Olmo na ina ombi la pauni milioni 40 ambalo litagawanywa kwa malipo ya miaka minne pamoja na nyongeza ya pauni milioni 20 kwa ajili ya kusamjili mchezaji huyo. (Mundo Deportivo – in Spanish)
SOMA: Man City yahamia kwa Alphonso Davies
Hata, Leipzig imekataa ofa ya Barcelona kumsajili Olmo kwa sababu ipo chini ya kiwango ilichotarajia. (Sky Sports Germany)
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ametabiriwa kuondoka RB Leipzig msimu huu wa kiangazi baada ya kuwa na mafanikio ya timu ya taifa na ameonesha kuvutia miamba kadhaa ya Ulaya.
Barcelona imekuwa ikijaribu kufanya majadiliano ya kumsajili Olmo na mchezaji mwenzake wa timu ya taifa, Nico Williams, baada ya Euro 2024 lakini bado haijakamilisha dili lolote wakati ikijaribu kutafuta muundo mzuri wa malipo.
Klabu hiyo ya Nou Camp inakabiliwa na uwezekano wa kuhitaji kuuza wachezaji ili kupata pauni milioni 50 ambazo kipengele cha zamani kumwachia Olmo kilikuwa kimeainishwa, na upande wa Bundesliga unatarajiwa kuwa wazi kumuuza kwa ada hiyo hiyo.
Hata hivyo, Man City haikabiliwi na ukomo huo wa kifedha na sasa inajaribu kuishinda Barcelona kumsajili Olmo, ambaye bado hajafanya maamuzi ya dhati kuhusu mustakabali wake.
Katika tetesi nyingine beki wa Everton Jarrad Branthwaite, 22, anakusudia kutosaini mkataba mpya katika klabu yake hadi itakapoweka dau inayolingana na ofa ya Manchester United ya pauni 160,000 kwa wiki. (Mail)
Mlinzi wa Manchester United Aaron Wan-Bissaka, 26, amekataa ofa ya awali ya West Ham na angependa kuhamia Inter Milan majira haya ya kingazi. (Talksport),
Crystal Palace imekubali kimsingi dili la pauni milioni 12.6 kumsajili winga wa Senegal Ismaila Sarr, 26, toka klabu ya Marseille. (Athletic – subscription required)
Arsenal imefungua mazungumzo na Paris Saint-Germain kuhusu kiungo wa Hispania Fabian Ruiz, 28, lakini uhamisho wa wa mchezaji huyo utahitaji The Gunners kumpa kwaheri mchezaji mmoja. (Football Transfers)