Manchester City kufukuzwa mashindano yote

KLABU ya Manchester City imeripotiwa kukabiliwa na kufukuzwa kwenye mashindano yote sio Ligi Kuu England pekee iwapo itapatikana na hatia ya kuvunja kanuni za fedha. Kwa mujibu wa gazeti la The Telegraph kesi inayohusu makosa 115 ya Manchester City kuvunja kanuni za Ligi Kuu England imeanza kusikilizwa wiki hii huku klabu hiyo ikituhumiwa kwa matumizi yasiyo sahihi ya fedha kwa miaka 9 kuanzia 2009.