Marekani, Ukraine kusaini mkataba wa madini maliasili

WASHINGTON DC: RAIS Donald Trump amesema kuwa Marekani inatarajia hivi karibuni kufikia makubaliano na Ukraine ili kusaini mkataba wa madini na maliasili.

Trump aliongeza kuwa juhudi za kutafuta makubaliano ya amani kati ya Urusi na Ukraine zimefikia hatua nzuri baada ya mazungumzo aliyofanya hivi karibuni na marais Vladimir Putin wa Urusi na Volodymyr Zelensky wa Ukraine.

Wakati huu, viongozi wa mataifa ya Ulaya wamekubaliana kuongeza matumizi yao katika sekta ya ulinzi kwa kutenga euro bilioni 800 ifikapo mwaka 2030. Vilevile, wamekubaliana kuongeza msaada wa kijeshi kwa Ukraine ili iendelee kukabiliana na uvamizi wa Urusi.

Advertisement

SOMA: Marekani kusitisha misaada ya kijeshi Ukraine

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *