Marufuku kula msibani

SIMIYU; Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk Yahaya Nawanda, amepiga marufuku watu kula kwenye misiba, kutokana na kuibuka tena kwa ugonjwa wa kipindupindu katika Wilaya za Meatu, Bariadi na Itilima.


Hiyo ni mara ya pili kwa mkoa huo kukumbwa na mlipuko wa ugonjwa huo, ambapo mara ya kwanza ilikuwa Desemba, 2023 hadi Januari, 2024 na kusababisha uwepo wa wagonjwa 273 huku vifo vikiwa vitatu.

Akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa huo, Dk Nawanda ameagiza kuanza kutekelezwa kwa mara nyingine marufuku ya watu kula misibani, kwani katika awamu ya pili ya mlipuko wa ugonjwa huo chanzo kikubwa imeonekana kuwa ni misiba.

“ Awamu ya kwanza tulipiga marufuku na tukafanikiwa kudhibiti ugonjwa huu, sasa umerudi tena, naagiza hapa tunasitisha tena watu kupika na kula misibani, imeonekana misiba imekuwa chanzo kikubwa cha ugonjwa huu,” amesema Dk Nawanda n kuongeza:

“ Tukimaliza kuzika kila mtu nyumbani, hakuna kupika wala kula kwenye misiba, awamu hii ya pili ugonjwa umekuja kwa kasi hasa Wilaya ya Meatu, na wote walipatwa na ugonjwa huu wameutoa misibani baada ya kula chakula.”

Mganga Mkuu wa Mkoa Dk Boniphace Marwa, amesema kuwa mlipuko wa awamu ya kwanza mkoa ulifanikiwa kuudhibiti, ambapo uwepo wa marufuku ya kula misibani na kufungwa kwa minada ilisaidia kwa kiasi kikubwa.

Habari Zifananazo

Back to top button