Mashabiki 13,000 Morocco wapewa tiketi za bure

Sawa Morocco kafungwa ila hadaiwi!

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu la Morocco, limetoa tiketi za bure 13,000 kwa mashabiki wa nchini humo kwa ajili ya nusu fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa kesho.

Morocco imeweka rekodi ya kuwa nchi ya kwanza Afrika kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Dunia, baada ya kuifunga Ureno katika Robo Fainali kwa 1-0 Uwanja wa Al Thumama jijini Doha, Qatar.

Bao pekee la Morocco maarufu kama Simba wa Atlasi , lilifungwa na Youssef En-Nesyri, dakika ya 42. Ufaransa imetinga Nusu Fainali baada ya kuichapa  England mabao 2-1.

Advertisement

 

 

/* */