Mashtaka mapya yamkabili Diddy
MAREKANI : ZAIDI ya watu 100 wanatarajiwa kumshtaki mwanamuziki wa rap Sean ‘Diddy’ Combs kwa unyanyasaji wa kingono, ubakaji na kutumiwa vibaya kingono .
Wakili Texas,Tony Buzbee aliwaambia waandishi wa habari kuwa baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa waathirika ni pamoja na watoto wadogo ambao walinyanyaswa walipokuwa na umri wa miaka tisa.
Wakili anayemwakilisha Combs, Erica Wolff alisema rapa huyo amekanusha madai hayo na kusema madai ni ya uongo na yenye lengo la kumuharibia sifa.
Wakili Buzbee aliwambia waandishi kuwa yeye na timu yake watafanya kila liwezekanalo kuwapata wahusika katika madai ya unyanyasaji ikiwa mtu yeyote au taasisi yoyote ambayo ilishiriki au kufaidika na tabia hiyo kuwafikisha katika mkono wa sheria.
Wolff ambaye ni wakili wa Combs anatarajia kuthibitisha kuwa mteja wake hana hatia na atajithibitisha mahakamani, ambapo ukweli utaelezwa kwa kuzingatia ushahidi, na sio uvumi.
Combs alikamatwa wiki iliyopita akikabiliwa na mashtaka ya uhalifu ya ulanguzi wa ngono na biashara ya ngono.
SOMA : Afungwa jela maisha kwa kulawiti hadharani
Kwa sasa yuko chini ya ulinzi baada ya kunyimwa dhamana, ambayo amepanga kukata rufaa.
Mpaka sasa Combs amekanusha madai yote ya uhalifu.