Mataifa 68 kuwekewa ushuru mpya

MAREKANI : RAIS wa  Marekani, Donald Trump, amesaini amri ya kuweka ushuru mpya kwa mataifa 68 pamoja na Umoja wa Ulaya, hatua inayotarajiwa kuanza kutekelezwa rasmi Agosti 7 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Afisa Mwandamizi wa Marekani aliyezungumza na vyombo vya habari kwa masharti ya kutotajwa jina, amesema kuchelewa kwa utekelezaji huo ni kutaka kutoa muda zaidi wa kuoanisha viwango vya ushuru kwa nchi husika.

Kwa mujibu wa amri hiyo, nchi za Umoja wa Ulaya zitawekewa ushuru wa asilimia 15, huku mataifa mengine yasiyo kwenye orodha hiyo yakikabiliwa na ushuru wa asilimia 10. SOMA: Trump kutangaza ushuru wa 25% kwa biashara ya chuma na aluminium

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button