Matola arejeshwa Simba
KLABU ya Simba imetangaza kuboresha programu za vijana kwa kuwateua meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu kuwa mkuu wa programu za vijana sambamba na teuzi ya Selemani Matola kuwa Kocha Mkuu wa timu za vijana.
Akizungumza na vyombo vya habari leo Mei 31, 2023 Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba Imani Kajula amesema Simba imedhamiria kuboresha programu za vijana ikiwa ni muendelezo walichokuwa wakikifanya miaka 11 iliyopita
“Simba inaamini kwa dhati kabisa ili kuwa na timu imara ni lazima tuwe na timu imara za vijana, kama ilivyomtoa Jonas Mkude na Hamis Ndemla waliotoka kwenye programu za vijana.” Imani Kajula.
Kwa upande wake Rweyemamu amesema ili mpira uweze kuendelea ni lazima kuimarisha timu za vijana
“Takribani wachezaji 250 tumewakuza katika programu za vijana na naweza kusema hakuna timu yoyote nchini katika ngazi zote ambayo haijanufaika na mchezaji kutoka kwenye timu za vijana za Simba” Patrick Rweyemamu.
Kwa upande wake kocha mkuu wa program hiyo ya vijana Seleman Matola amesema imekuja kwenye wakati sahihi
“Sintaiangusha bodi sintaiangusha klabu ya Simba.” Selemani Matola
Simba wanalenga kuwa na timu bora ya baadae kupitia uwekezaji wa kwenye soka la Vijana ambapo wanaenda na kauli mbiu isemayo wakati ujao ni sasa.