WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umeanza kutoa mafunzo ya namna ya kutumia mifumo ya kufuatilia wa viashiria na matukio ya moto kwa kutumia njia ya mtandao kupitia setelaiti ambayo yatawawezesha wahifadhi kuchukua hatua za haraka za kudhibiti wakishirikianana wadau wengine .
Ofisa Uhifadhi Mwandamizi wa Wakala huo, Rogers Nyinondi kutoka makao makuu amesema hayo wakati wa utoaji mafunzo kwa wahifadhi kutoka Kanda ya Mashariki na kufanyika mkoani Morogoro.
Nyinondi ambaye ni mtaalamu wa kitengo cha ufuatiliaji na matukio ya moto msituni amesema kutokana na kujengewa uwezo huo, wahifadhi wapata ujumbe wa matukio ya moto kwenye maeneo yao wanayoyasimamia kupitia simu za kiganjani (Simu Janja).
SOMA: Wananchi waahidi ulinzi uchomaji misitu
Amesema njia hiyo ni kuyapata kwa uharaka matukio hayo na kubaini viashiria vya moto na kutawarahisishia kudhibiti na kuyafikia matukio ya moto kwa haraka zaidi na kuuzima.
Nyinondi amesema mafunzo hayo ni sehemu ya kwanza ya mpango wa muda mrefu ambayo watapewa wahifadhi wote wa Wakala huo nchi ili kuwawezesha kukabiliana na matukio ya moto na kubaini viashiria vya moto kwenye maeneo yao na kuchukua hatua za udhibiti.
“ Mafunzo haya ni sehemu ya kwanza kutolewa na TFS kwa wahifadhi wa wilaya ,mashamba ya miti na hifadhi ya msitu asilia wa Kanda ya Mashariki lakini baadaye yataendelea maeneo mengine ya nchi,” amesema Nyinondi.
SOMA: Samia aonya uchomaji misitu
Nyinondi amesema lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuhakikisha matukio ya moto yanathibitiwa pale yanapotokea na pia katika kufuatilia viashiria vya moto kabla haujatokea na kuchukua tahadhari.
“Ni mifumo rafiki ,kinachotakiwa ni kuwa na simu janja na kutumia mtandao na kuweza kungia na kuona matukio ya moto maeneo mbalimbali na hata kama upo jirani na hivyo kuchukua tahadhari mapema” amesema Nyinondi.
Amesema TFS itaendelea kuwafundisha wataalamu wake ambao nao watawafikia wananchi na kuwafundisha mifumo hiyo ambayo itawasaidia watu kuchukua tahadhari ya baadaye .
Ofisa Mhifadhi, Zarina Shaweji kutoka Hifadhi ya Mazingira ya Asili Uluguru,amesema mafunzo waliyopata ya kutumia setelaiti kwa kutumia mtandao ya kutambua ama kupata vashiria vya moto unaotokea msituni yamekuwa ya muhimu.
Shaweji amesema njia hiyo inawezesha wahifadhi hata wanapokuwa nje ya misitu lakini kwa kutumia setelaiti kutawawezesha kutambua mioto inayotokea ndani ya msitu kwa kupata ujumbe katia simu kupitia mifumo hiyo.
“ Mafunzo haya ni mazuri na tunaishukuru taasisi kwa kutujengea uwezo tukiwa watumishi namna ya kukabiliana na mioto ambayo inatokea msituni,” amesema Shaweji.