RAIS Samia Suluhu Hassan amewaonya wananchi kuacha tabia ya kuchoma misitu, kinyume chake wailinde na kuihifadhi.
Kiongozi huyo wa nchi ametoa onyo hilo leo Septemba 26, akiwa katika Wilaya ya Namtumbo Mkoa wa Ruvuma wakati akizungumza na wananchi katika muendelezo wa ziara yake.
SOMA: Kilimo kuwa chanzo kikubwa pato la taifa
“Acheni kuchoma misitu moto na kama ni lazima uchome moto shamba linda moto usitapakae kwenda kuharibu maeneo mengine ya misitu yaliyohifadhiwa,” amesema Rais Samia.