Matunda kampeni ya kumtua Mama ndoo kichwani

MTWARA: SERA ya kumtumia Mama Ndoo Kichwani imewezesha upatikanaji wa maji safi na salama kwa asilimia 100 katika vijiji vyote saba vilivyopo katika Kata ya Mkundi, Wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtwara.

Diwani wa Kata ya Mkundi, Twahili Ntima amesema serikali imejenga miradi ya maji safi na salama ambayo imewezesha vijiji vyote maji ya kudumu na kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji katika kata hiyo.

“Zaidi ya miaka ishirini tulikuwa hatupati maji safi na salama, asilimia kubwa ya wananchi walikuwa wanatembea umbali wa kilomita nane kwenda kupata maji, weng wakienda kando ya Mto Ruvuma, sehemu ambayo ilikuwa ikihatarisha maisha yao,”.

SOMA: Rais Samia amedhamiria kumtua Mama ndoo kichwani

Diwani huyo amesema kuanzia mwaka 2022, serikali ilisikia kilio cha wananchi katika kata hiyo na kuanza kupeleka miradi ya maji ambayo ilikuwa na sera ya Kumtua Mama Ndoo Kichwani.

“Mwaka 2022 kwa mara ya kwanza, serikali ilituletea mradi ambao ulipelekwa kwenye vijiji vya mpakani na nchi ya Msumbiji, ukawa ukoombozi kwa baadhi ya wananchi hasa akina mama ambao ndiyo walikuwa waathirika zaidi,” amesema.

Amesema Kampeni ya Kumtua Mama Ndoo Kichwani iliyoanzishwa na Raisi Dk Samia Suluhu Hassan imekuwa chachu katika kuharakisha utekelezaji wa mradi na baadae Mwaka 2023 serikali ikaongeza miradi mingine.

Ntima amesema hayo mara baada ya Mwenge wa Uhuru kutembelea na kukagua mradi wa maji wenye thamani ya Sh bilioni 1.4 katika Kata ya Mkundi, Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara.

Mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka mwezi Januari mwaka huu umelenga kutoa huduma ya maji kwa wananchi 10,947.

Habari Zifananazo

Back to top button