Maendeleo ukarabati Mv Liemba yaelezwa bungeni

DODOMA; Serikali imesema meli za Mv Liemba na Mv Mwongozo zitaanza kutoa huduma za usafiri katika ziwa Tanganyika baada ya ukarabati wa meli hizi kukamilika.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Bazilio Kapunda aliyehoji ni lini meli hizo zitaanza kutoa huduma zake ndani ya Ziwa Tanganyika.
‘’Kwa sasa ukarabati wa Mv Liemba unaendelea na kwa sasa upo katika hatua ya ufungwaji wa vifaa muhimu baada ya kupokelewa na inatarajiwa kukamilika matengenezo hayo mwezi wa Juni, 2026 na kukabidhiwa kwa TASHICO mwezi Julai, 2026 kwa ajili kuendelea kutoa huduma za usafirishaji ndani ya ziwa Tanganyika.
‘’Aidha taratibu za kuanza ukarabati mkubwa wa Mv Mwongozo unaendelea kukamilishwa ili kuanza matengenezo hayo hivi karibuni,” amesema naibu Waziri.



