Vipaumbele 8 bajeti ya ulinzi mwaka 2026/27

DODOMA; Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk Rhimo Nyansaho amewasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ikiwa na vipaumbele 8.

Akiwasilisha bungeni hotuba hiyo leo Mei 19, 2026, ametaja vipaumbele hivyo ni kuliimarisha jeshi kwa zana na vifaa vya kisasa, kiteknolojia, mawasiliano na rasilimali watu;

“Kuendelea kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi kwa wanajeshi ikiwemo kutunza vifaa na zana, mazoezi, mafunzo, maslahi, huduma za afya na makazi;

“Kuendelea kuimarisha uwezo wa Jeshi la Kujenga Taifa kwa kuboresha miundombinu, ili liweze kuchukua vijana wengi zaidi watakaopata mafunzo ya awali ya kijeshi na stadi za kazi;

“ Kuendelea kuliimarisha Jeshi la Akiba; kuendeleza na kulinda miradi ya kimkakati kwa maslahi mapana ya Taifa;, Kuimarisha mashirika na taasisi za utafiti wa masuala ya kijeshi.

“Kuanzisha viwanda vipya katika Sekta ya Ulinzi (Defence industries) vitakavyozalisha bidhaa kwa matumizi ya Kijeshi na Kiraia. Pia, kuanzisha viwanda vipya kwa kushirikiana na Sekta Binafsi;


“Kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki na kati ya Nchi na Nchi katika masuala ya ulinzi; na

“Kuendelea kushirikiana na Mamlaka za kiraia katika kukabiliana na majanga na dharura inapohitajika,” amesema Waziri huyo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button