WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde amezindua mnada wa kwanza wa ndani wa madini ya vito katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro, Mkoa wa Manyara.
Kwa mujibu wa Wizara ya Madini, gramu 184.06 za madini mbalimbali ya vito yenye thamani inayokadiriwa kufikia shilingi bilioni 3.1 yanatarajiwa kuuzwa kupitia mnada huo.
Mnada huo unaendeshwa kwa njia ya kidigitali na hivyo kutoa nafasi kwa wafanyabiashara wa madini kutoka maeneo mbalimbali nchini kushiriki kupitia njia ya mtandao.