Mawasiliano kuboreshwa hospitali ya Temeke

DAR ES SALAAM :WIZARA ya Afya imeahidi kuboresha maeneo yatakayoimarisha huduma za afya kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke.

Maeneo hayo ni huduma kwa wateja (Customer Care) na changamoto ya mawasiliano kutoka kitengo kimoja kwenda kingine

Hayo ameyasema leo Agosti 26 jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, John Jingu alipofanya ziara hospitalini hapo kuangalia ubora wa utoaji huduma.

SOMA:Magonjwa yasiyoambukiza tishio Temeke

“Tumekutana na wagonjwa kuona ni namna gani wanapokea huduma zetu na kiwango kikubwa wagonjwa wanasema wanaridhika na huduma ambazo tunazitoa si tu kama wanasema na me nimejionea na msafara wangu katika kuzunguka kote huku,”

“Kuna maeneo ambayo tunahitaji kuyafanyia kazi ili kuimarisha utoaji wa huduma kwa ufanisi lakini kwa tija zaidi eneo la huduma kwa wateja (Customer care) tunataka mtu akija hapa basi apate huduma mara moja asikae zaidi ya muda uonahitajika kukaa lakini pia kuna changamoto zingine za mawasiliano kutoka kitengo kimoja kwenda kingine na yenyewe inaweza kuleta ucheleweshaji wa hapa na pale lakini tunawekeza kwa kiwango kikubwa kwenye tehama itasaidia kwa kiasi kikubwa ucheleweshaji huu,”amesema Jingu.

SOMA: Wanafunzi Sudan kuhamishiwa hospitali ya Temeke

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Joseph Kimaro amesema ziara hiyo inawapa motisha wao watumishi walio chini ya Wizara ya Afya kuendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi wanaozitegemea.

Habari Zifananazo

Back to top button