Mawaziri watakiwa kutenga muda kero za wananchi

DODOMA; Waziri Mkuu Dk Mwigulu Nchemba, amewataka mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya kutenga muda wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi hususan migogoro ya ardhi.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo kwenye hotuba yake yak kuahirisha shughuli za Bunge la 13 Mkutano wa Pili ulioanza Januari 27, 2026.

“Niendelee kuwasisitiza mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na Watumishi wa umma watenge muda wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika maeneo yao hususan kwenye migogoro ya ardhi.

“Wafuateni, wasikilizeni na tatueni kero zao, ili wasilazimike kwenda ngazi za juu au kusubiri ziara za viongozi wa kitaifa kwa masuala ambayo mngeweza kuyafanyia kazi,” amesema Waziri Mkuu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button