Mbarawa: kufikia 2025 tutakuwa na Ndege 16

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa kesho Oktoba 03, 2023 Tanzania inatarajia kupokea ndege mpya ya abiria (Boeing 737 max9) kutoka nchini Marekani yenye uwezo wa kubeba watu 181, mizigo tani sita na uwezo wa kuruka kwa saa 8 bila kutua.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam, katika mkutano na waandishi wa habari, ambapo ameeleza kuwa pamoja na kupokea ndege hiyo pia watakabidhi ndege mbili za mafunzo kwa Chuo cha Usafirishaji (NIT) zenye uwezo wa kubeba watu wanne kwa ajili ya mafunzo ikilenga kuongeza wataalamu wa ndani kuzihudumia ndege hizo.
Aidha, Kiongozi huyo ametanabaisha kuwa kufikia mwaka 2025 Tanzania itakuwa na jumla ya ndege 16 jambo ambalo litaongeza wigo katika sekta ya Utalii na biashara kwa lengo la kukuza pato la Taifa.
Itakumbukwa kuwa safari hii ya mafanikio ilianza mwaka 2016 katika harakati za kulifufua Shirika la Ndege nchini (ATCL), ambapo mpaka kufikia leo tayari zipo ndege 13.
ATCL kwa sasa linahudumia vituo vya ndani 14 na vingine vya nje vikiwemo Entebe, Kenya, Burundi, Comoro, Zimbabwe, Mumbai na China.
Google paid 99 dollars an hour on the internet. ( a44q) Everything I did was basic Οnline work from comfort at home for 5-7 hours per day that I got from this office I found over the web and they paid me 100 dollars each hour. For more details
visit this article————>> http://Www.SmartCareer1.com
HE/SHE DIED WITH CARDINAL RUGAMBWA HOSPITAL “CONFERENCE” DISEASE… THE HISTORY OF THIS DISEASE WAS KILLED MORE THAN 5 MILION PEOPLE AROUND THE WORLD MANY WAS CHINESE, EROPEAN, KOREAN AND INDIANS… ALL WHERE WHITE SKIN PEOPLE