Mbeya yakusanya bil 2.3/- madini

MKOA wa Mbeya umekusanya jumla ya Sh bilioni 2.3 sawa na asilimia 63 ya lengo la mwaka kati ya Julai 2024/ 2025 ikiwa ni makusanyo ya maduhuli ya serikali yanayotokana na mrabaha, tozo na ada mbalimbali katika Sekta ya Madini.

Akizungumza kwa niaba ya Ofisa Madini Mkazi, Mkoa wa Mbeya, mhandisi migodi, William Kajumla amesema Mkoa wa Mbeya ulipangiwa kukusanya Sh bilioni 3.7.

Amesema mapato makubwa katika Mkoa wa Mbeya yanatokana na madini ya viwandani, dhahabu na madini ujenzi, pamoja na mapato katika miradi mbalimbali ya barabara.

Advertisement

“Tunategemea mapato kutoka kwenye kiwanda kinachozalisha hewa ya ukaa cha TOL Gas Rungwe na Kiwanda cha Saruji Mbeya kwa madini ya viwandani lakini pia, biashara ya dhahabu na machimbo madogo madogo ya madini ujenzi,” amesisitiza.

Kajumla alitoa wito kwa Watanzania kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo katika Mkoa wa Mbeya hususani sekta ya madini ujenzi, makaa ya mawe Ngana Kyela na Rungwe na fursa za uwekezaji kwenye uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu kwenye maeneo ya Mabadaga, Msesule na Madibira wilayani Mbarali na Lwanjiro, Ileya, Ishinda na Chikula wilayani Mbeya.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *