Mbunge aanzisha mfuko maalumu kusaidia wanafunzi Ngorongoro

ARUSHA: Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro mkoani Arusha, Yannick ameanzisha mpango maalumu wa kuanzisha mfuko wa elimu utakaowanufaisha wanafunzi 280 kutoka wilayani Ngorongoro wanaotoka katika familia zisizo na uwezo wa kuwapeleka sekondari.

Hatua hiyo ni katika kuunga mkono juhudi za Serikali kusukuma mbele ajenda ya elimu bure kuanzia darasa la awali hadi kidato cha sita.

Hatua hiyo imekuja kufuatia changamoto kubwa ya kipato inayowakabili wakazi wengi wa Wilaya ya Ngorongoro, ambao kwa kiasi kikubwa hutegemea ufugaji kama chanzo chao kikuu cha maisha.

Katika kutekeleza azma hiyo, Ndoinyo ameitisha kikao maalumu kilichowakutanisha wadau wa maendeleo ya elimu, wakiwemo makampuni ya utalii, taasisi za fedha pamoja na mashirika ya umma, kwa lengo la kujadili na kuanzisha rasmi mfuko huo wa elimu.

Lengo kuu likiwa ni kuhakikisha wanafunzi wanaojiunga na elimu ya sekondari kutoka familia duni wanapata mahitaji muhimu ya kuanzia safari yao ya elimu  bila vikwazo vya kifedha.

“Wazo hili lilianza mwaka 2025 nilipochaguliwa kuwa mbunge. Nilipokea maombi mengi kutoka kwa wazazi waliokuwa na changamoto ya kuwapeleka watoto wao shule. Nilianza kwa kusaidia wanafunzi 80  wavulana 40 na wasichana 40  na hapo ndipo nikatambua hitaji ni kubwa zaidi,” amesema.

Mbunge alisema kuwa mfuko huo si tu msaada wa vifaa, bali ni uwekezaji wa moja kwa moja katika mustakabali wa Taifa katika kukuza elimu kwa jamii zote za watanzania .

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Mohamed Hussein, akimuwakilisha waziri wa Elimu, amesema serikali tayari imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu.

Ametaja ajira za walimu zaidi 20, 000 ujenzi wa madarasa zaidi ya 30,000 pamoja na mabweni kwa wanafunzi kutoka jamii za wafugaji, kuwa ni sehemu ya juhudi hizo za serikali.

“Tunampongeza Mbunge wa Ngorongoro kwa kuunga mkono jitihada za serikali. Huu ni mfano wa utekelezaji halisi wa sera ya elimu na mchango muhimu katika kuimarisha upatikanaji wa elimu bora.” alisema Hussein

Nao viongozi wa wilaya hiyo wameahidi kusimamia mfuko huo kwa uwazi na uwajibikaji wa hali ya juu.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Manja Yaile, amesema watahakikisha kila mchango unamfikia mlengwa aliyekusudiwa na kuhakikisha mfuko unakuwa na kila anayechangia ataona matokeo yake kwa wanafunzi.

Zaidi ya hapo, mfuko huo unatarajiwa kuwa daraja la fursa kwa vijana ukisaidia pia kuwaunganisha na nafasi mbalimbali kama ufadhili wa masomo kupitia programu kama Samia Scholarship.

Yaile alisema mfuko huu hauishii kwenye sare, madaftari au vifaa vya shule pekee  bali unapanua wigo wa ndoto kwa vijana wa Ngorongoro kupata elimu kwani dunia ya leo, elimu si chaguo  ni silaha na wilaya ya Ngorongoro, kupitia mfuko huu, inaanza kuandaa kizazi kitakachobadilisha simulizi ya kesho.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I make over 13k a month working part-time. I listened to different humans telling me how a good deal of cash they may make online,N255 so I was detedrmined to locate out. Well, it turnded into all actual and it absolutely modifiedd my life. Everybody must try this job now by just
    using this site….>>>> w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

  2. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  3. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button