Mchengerwa kuongoza Tamasha la #Sensabika
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohammed Mchengerwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la kuhamasisha Sensa la #Sensabika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Hassan Abbasi mapema leo amewaongoza mamia ya wadau wa utamaduni, sanaa na michezo kuianza Siku ya Tamasha la Kuhamasisha Sensa la #Sensabika kwa mazoezi.
Tamasha hilo linaendelea mchana huu kwa muziki na ngoma na michezo mbalimbali na jioni kutakuwa na pambano la ngumi la bondia Karim Mandonga na kisha wasanii wakubwa chini watapanda stejini.