Mfalme Abdullah II akataa pendekezo la Marekani

JORDAN : MFALME Abdullah II wa Jordan amekataa pendekezo la Marekani la kutaka kuwahamisha Wapalestina, baada ya mazungumzo na Rais Donald Trump wa Marekani, ambaye alishauri wakazi wa Gaza wapatao milioni 2 kuondolewa kutoka katika eneo lililoharibiwa na vita.

Katika mkutano na Rais Trump, Mfalme Abdullah alijitolea kuchukua hadi watoto 2,000 kutoka Gaza, hasa wale wanaohitaji matibabu ya dharura, ikiwemo watoto wa saratani.

Kupitia mtandao wa X, Mfalme Abdullah alisema, “Msimamo wa Jordan ni msimamo wa pamoja wa mataifa ya Kiarabu.” SOMA: Marekani yajipanga kuchukua udhibiti Gaza

Advertisement

Vilevile, Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit, alikosoa pendekezo hilo, akisema kuwa ni lisilokubalika katika ukanda huo, huku China ikisisitiza kuwa Gaza ni ardhi ya Wapalestina.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *