Mfumo kudhibiti vifo vya uzazi wazinduliwa Dar

Programu hiyo imezinduliwa kupitia mradi wa “10 milioni safe birth initiative” utakaotekelezwa katika mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam kwa kipindi cha mwaka 2025 hadi 2027.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Wizara ya Afya, Ziada Sellah amesema mradi huo umekuja wakati sahihi kwasababu mkunga anaweza kujifunza mahali popote pale akiwa kazi, nyumbani hata kama hamna mtandao akishapakua anafungua kawaida.
“Akipata changamoto anaweza kuona nini cha kufanya kupitia hiyo na kama application iliyozinduliwa leo tuna magroup ya WhatsApp na inawezekana mkunga yuko Rufiji akapata changamoto anaeleza kwenye hayo magroup ili wapate msaada.
Amebainisha kuwa ili kuwafikia wakunga zaidi wana waratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto katika halmashauri na kupitia hao waratibu pamoja na wakunga wakuu wa mikoa pamoja na halmashauri watakwenda kujengewa uwezo huko chini.
“Na kwasababu unatakiwa kuwa tu na simu janja akiwa nayo itakuwa inamuelekeza anachokihitaji .
Kwa upande wake Dk Beatrice mwilike, Mkunga Bingwa na Rais wa Chama cha wakunga Tanzania (TAMA) amesema
Kupitia mradi huo wao wanasehemu kubwa katika kutoa mafunzo kwa wakunga ili kutumia hiyo app na kuwaunganisha katika mafunzo na kuwaongezea weledi.
“Kwa kushirikiana na UNFPA na Maternity Foundation tunanafasi ya kuhakikisha wakunga wote wanafikiwa ili kuweza kujifunza wanayotakiwa kufanya wanapotoa huduma kwa mama na mtoto au wanapotoa elimu ya uzazi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Training Center for International Health (TTCIH) Edward Amani amesema katika mradi huo wa 10 milioni safe birth initiative wanaratibu shughuli zote zilizopangwa kufanyika kwa wakati na zinapata fedha kwa wakati.
“Tutakuwa na jukumu la kujua kipi kinafanyika,kipi bado na kinafanyika lini na mradi huu umewekeza kwa wakunga kutoa huduma salama kumfanya mama na mtoto wawe hai
Mratibu Miradi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA),
Sunday Rwabagira amefafanua kuwa wanakusudia kuongeza upatikanaji wa wakunga wataalamu zaidi na wanafanya mradi huu kwa nchi nane zilizpo kusini mwa jangwa la Sahara kwa ufadhili wa serikali ya Denmark.
“Katika mradi huu tunalenga uzazi salama kwa watoto milioni 10 ifikapo 2030 wakunga watatumia njia za kisasa zitakazowapa taarifa sahihi.
Balozi wa Denmark nchini Jesper Kammersgaard amesema serikali yake imetoa kiasi cha Sh Bilioni 11 kuweza kufanikisha mradi huo kupitia Taasisi ya Maternity Foundation kwa kushirikia na UNFP na Wizara ya Afya .
“Mradi utakuwa kuanzia mwaka 2025 hadi 2027 itasaidia kupunguza vifo vya uzazi zaidi kulingana na malengo ya millennium,”amesisitiza.