Mhagama atoa maagizo kwa halmashauri zote

WAZIRI wa Afya, Jenista Mhagama amezitaka halmshauri zote nchini kutenga fedha za utekelezaji wa afua za lishe, uongezaji wa virutubisho kwenye vyakula ili kubaini matatizo ya utapiamlo na viribatumbo na magonjwa yasiyoambukiza.

Waziri Mhagama ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Maadhimisho ya Siku ya Lishe Kitaifa yanayoadhimishwa Oktoba 30 kila mwaka yenye kauli mbiu isemayo “Mchongo ni Afya yako, zingatia unachokula “kwa lengo la kuongeza uelewa wa jamii kuhusu manufaa ya lishe bora na hatua chanya zinazochukuliwa ngazi za jamii.

SOMA: Wizara ya afya yaingia ushirikiano afya ya uzazi

Amesema endapo kila halmashauri zikitenga fedha hizo zitawezesha kusaidia jamii kupata elimu na uelewa zaidi ngazi ya kata,mashuleni ili kupunguza tatizo la utapiamlo na kupata jamii bora kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii .

Amesema jamii bado inakabiliwa na changamoto ya utapiamlo wa aina zote tatu ikiwemo ukondefu,udumavu, uzito pungufu hususan kwa watoto , utapiamlo wa upungufu wa vitamini na madini mwilini yani njaa iliyofichika , upungufu wa damu, utapiamlo wa lishe ya kuzidi ,kiribatumbo pamoja na magonjwa yasiyoambukiza.

Habari Zifananazo

Back to top button