Mhariri TSN ashinda uenyekiti Taswa

MHARIRI wa habari za Kiswahili za kidigiti wa kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) Amir Mhando amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa) katika uchaguzi mkuu uliofanyika Dar es Salaam jana.

Mhando ambaye katika uongozi uliomaliza muda wake alikuwa Katibu Mkuu alipata kura 57 na mpinzani wake Mbwana Shomari akiambulia kura 11 katika kura 68 zilizopigwa.

Alfred Lucas alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu kwa kura 57, Issa Ndokeji akipata kura 9 huku kura mbili zikimkataa na Michael Noel akiambulia patupu.

Mwanadada Imani Makongoro alichaguliwa Katibu Msaidizi kwa kura zote 68, Dina Ismail alichaguliwa kuwa Mweka hazina kwa kura 65 na wajumbe wa kamati ya utendaji ni Timzoo Kalugira aliyepata kura 62 na Nasongelya Kilyinga kwa kura 60.

Akizungumza baada ya kutangazwa na kuapishwa Mhando aliwashukuru wajumbe kwa imani waliyoonesha kwake na viongozi wenzake na kuahidi kufanyia kazi changamoto zote ili kurejesha hadhi ya Taswa.

“Nyoka anauwawa kwa jina lake lakini wengine hawana sumu ndivyo tasnia yetu inayoonekana wakati si wote hivyo tutahakikisha tunakumbushana kuhusu weledi na maadili ya kazi ili kurejesha heshima kwa jamii,” alisema.

Naye mlezi wa Taswa kutoka Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Charles Maguzo aliwataka viongozi kurejesha ushirikiano, kutoa kadi za wanachama na kufanya marekebisho ya katiba.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x