MAPUTO, Msumbiji: KATIKA historia ya nchi yetu, mnamo Agosti 29, 2024 ilitimia muongo mmoja, tangu Timu ya Serikali ya Tanzania ikwae ‘pipa’ kuelekea Maputo, Msumbiji kwenye kesi ya mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Malawi.
Katika timu hiyo alikuwemo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Mstaafu Frederick Werema, aliyezikwa jana Januari 04, katika Kijiji cha Kongoto, Wilaya ya Butiama Mkoa wa Mara.
Wajumbe wa Timu hiyo ya Serikali walikuwa saba ambapo Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Shamim Nyanduga alijumuika nao.
Kutoka kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari (Wakati huo akiwa ndani ya timu yawanasheria wa serikali).
Patrick Tsere, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi Deo Filikunjombe (aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ludewa) alikuwa kama shahidi kwenye timu hiyo.
Hayati, Benard Membe ndiye alikuwa Mkuu wa msafara huo wakati huo akihudumu nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje, alimjumuisha, Johari kwenye timu hii baada ya kuvutiwa sana na “Atikali Mujarab” aliyokuwa ameiandika gazetini kuhusu mgogoro huo.
Prof. Anna Tibaijuka aliyekuwa Waziri wa Ardhi.
Hayati, Fredrick Werema, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amefariki Desemba 30, 2024 akiwa kwenye matibabu, Hospitali ya Taifa Muhimbili akiwa na miaka 69.
Wa mwisho ni John Komba, aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Nyasa, katika msafara huo alikuwa ni shahidi.