TETESI za Usajili zinasema vilabu vya Chelsea, Manchester United, Bayern Munich na Paris Saint-Germain vimewasiliana na wakala wa kiungo wa Barcelona, Pablo Martín Páez Gavira maarufu Gavi, ambaye anakabiliwa na sintofahamu ya hatma yake baada ya kupata majeraha makubwa yaliomfanya akae nje ya dimba kwa muda mrefu. (El Nacional – Spain)
SOMA: PSG yahamia kwa Gavi
Wakati hatma ya Virgil van Dijk Liverpool ni kitendawili, timu hiyo imeweka orodha ya nyota wanne mbadala wake wakiwemo Gleison Bremer wa Juventus, Goncalo Inacio wa Sporting CP , Loic Bade anayekiwasha Sevilla na Marc Guehi wa Crystal Palace. (TEAMtalk).
Arsenal inataka kumsajili kiungo mpya kuchukua nafasi ya Thomas Partey mwaka 2025 na ipo tayari kumpeleka Emirates mlengwa wa usajili wa Liverpool Martin Zubimendi wa Real Sociedad. (TEAMtalk)
Manchester United ipo tayari kukamilisha mpango wa dili la kumsajili kiungo wa Norway Sverre Nypan, 17, wakati wa dirisha la uhamisho Januari 2025. (GIVEMESPORT)