Michezo ya majeshi sasa kimataifa

WIZARA ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ipo katika mazungumzo na viongozi wa majeshi kuona namna wanamichezo wao wanakuwa na nafasi kubwa kuliwakilisha taifa kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Naibu Waziri Hamis Mwinjuma amesema hayo jana katika hotuba aliyomwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika hafla ya kufunga mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA).

Michezo hiyo ilianza kutimua vumbi Septemba 6, katika viwanja mbalimbali vilivyopo mkoani Morogoro na kufikia tamati Septemba 15, mwaka huu.

Naibu Waziri amesema kwa mujibu wa Sera ya Michezo ya Taifa kuwa wanayo nafasi kuwashirikisha wanajeshi na wanausalama  katika kuchezo ili kujenga afya ya mwili na akili na kuwaleta pamoja.

SOMA: Michezo ya majeshi kuanza leo

Ameshauri majeshi hayo kuendelea kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo yenye dhamana ya michezo na mashirikisho ya vyama vya michezo nchini.

Amesema lengo ni kuweka taratibu ambazo zitawezesha majeshi yetu kuedelea kutoa wawakilishi wengi wanaoliwakilisha taifa kwenye mashindano mbalimbali ya  kimataifa.

“Katika hili tumeshalijadili sana na afande CDF na kwa kina,  na hivi karibuni tunaanza rasmi mazingumzo ramsi ya jinsi ya kuliendea jambo hili,” amesema Naibu Waziri Mwinjuma.

“…tunataka wanamichezo kutoka majeshini wawe na nafasi kubwa ya kuliwakilisha taifa kwenye mashindano ya kimataifa “ amesisitiza  Mwinjuma.

Naibu waziri amegusia pia suala la utaratibu wa upajikanaji wa mafunzo kwa walimu, viongozi na waamuzi ikiwa na kujenga viwanja vinavyofaa kwa michezo na jambo hilo liendelezwe katika majeshi yetu.

Pia ameshauri majeshi kuendelea kukuza program  kuendeleza michezo kwa vijana  na kuwa na mpango maalumu wa kuwatafuta hao vijana a michezo na wenye vipaji na wenye sifa ya kujunga na majeshi yetu ili wakati wote timu hizi ziwe na damu changa.

“ Kwa mipango tulioyonayo  timu zetu wakati wote zikiwa na damu changa inatuwezesha kuwatumia wakati fursa zinapopatikana,“ amesema Naibu Waziri.

SOMA: Kombe la Mkuu wa Majeshi Julai 20

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Salum Haji Othuman akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi na kwa niaba ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama ameyapongeza  majeshi hayo  kwa kuweza kuandelea  na kushiriki michezo hiyo  mkoani Morogoro licha ya kuwa na majukumu yao ya kuhakikisha nchi inakuwa salama.

“Majeshi yetu ni moja ya mihimili mikuu ya nchi yetu si kwa kuzingatia tuu ulinzi na usalama bali pia katika michezo kwa maana michezo huimarisha afya za wanajeshi ,kukuza uelewano na ushirikiano miongoni mwao na kukuza sekta ya michezo nchini, “ amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button