Mikakati kukabili ongezeko wagonjwa wa kansa yaelezwa

DODOMA; SERIKALI imesema inatekeleza mikakati mbalimbali kukabiliana na ongezeko la wagonjwa wa kansa.

Kauli hiyo imetolwa na Naibu Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Kisangi aliyehoji serikali ina mpango gani wa kudhibiti ongezeko la wagonjwa wa kansa nchini.

Naibu Waziri ametaja baadhi ya mikakati hiyo ni kutoa elimu kwa umma kuhusu kujikinga na ugonjwa wa saratani kupitia vipindi vya redio, televisheni, machapisho, magazeti na mitandao ya kijamii.

“Serikali inatoa chanjo ya (HPV) kwa wasichana ili kuwakinga na kirusi kinachosababisha saratani ya mlango wa kizazi.

“Kuanzisha huduma za awali za uchunguzi na matibabu ya saratani kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali za Taifa.

“Serikali imeimarisha huduma za kibingwa za uchunguzi na matibabu kwa kuhakikisha uwepo wa wataalamu na vifaa tiba kwa ajili ya kukabiliana na saratani,” amesema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button