Mikakati yatajwa maji shule zenye vyoo vya kisasa

MBUNGE wa Sikonge, Joseph Kakunda amehoji bungeni kuhusu utatuzi wa tatizo la kukosa huduma ya maji kwenye shule za msingi na sekondari zenye vyoo vya kisasa
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais (Tamisemi), Zainabu Katimba, amesema serikali inatambua kuwa kuna baadhi ya shule zenye vyoo vya kisasa kwenye shule za msingi na sekondari ambazo hazina huduma ya maji kutoka vyanzo vya uhakika.
“Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia Mamlaka za Maji Vijijini na Mijini zimeelelekezwa kuhakikisha kuwa taasisi za umma ikiwa ni pamoja na shule zinaunganishwa na mtandao wa maji katika maeneo yenye mtandao wa maji ya uhakika.
“Mikakati ya serikali ya kuhakikisha kuwa shule zinakuwa na vyoo vya kisasa vyenye huduma ya maji ni pamoja na; ujenzi wa shule mpya unajumuisha fedha za ujenzi wa miundombinu ya maji inayohusisha kuvuna maji ya mvua, kuunganisha na mifumo ya Mamlaka za Maji na kuchimba kisima;
“Ujenzi wa miundombinu ya vyoo unajumuisha fedha ya ujenzi wa miundombinu ya maji tiririka; na kutumia sehemu ya fedha ya ruzuku uendeshaji wa shule kukarabati kufanya ukarabati wa miundombinu ya maji,” amesema Naibu Waziri.