Mil 7/- kugombaniwa Mulalila Cup

JUMLA Sh milioni 7 zinashindaniwa katika mashindano ya mpira wa miguu ya Mulalila Cup ambayo yanajumisha jumla ya timu 18 kutoka Wilaya za Bukoba na Muleba lengo likiwa ni kuibua vipaji na kuleta burudani katika jamii.

Mashindano hayo yamefunguliwa katika uwanja wa Kagoma Wilaya ya Muleba na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa soka. Mashindano hayo yamefikisha miaka 10 tangu yalipofunguliwa mwaka 2015.

Mkurugenzi wa Mashindano hayo, Fortunatus Muhalila amesema mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha Sh milioni 5 na mshindi wa pili tajichukulia Sh milioni 2 huku akieleza kuwa  lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kukuza Vipaji ,kutoa elimu juu ya maswala ya uvuvi haramu.

Advertisement

“Kwa kipindi cha miaka 10 kwa sasa tunajivunia vijana wengi waliopitia ligi ya Muhalila Cup kucheza katika ligi zetu za Tanzania hasa Ligi Kuu ,na Ligi Daraja la Kwanza na la pili, baadhi ya vijana wako katika ligi kuu ya kenya ambapo wadau wa michezo wamekuwa wakifatilia mashindano hayo na kuchukua vijana kuendeleza vipaji,” amesema Muhalila.

Edo kumwembe ambaye ni mdau wa michezo alikuwa mgeni wa heshima katika ufunguzi wa mashindano hayo ametoa wito kwa vijana kuonyesha Vipaji vyao  na kufanikisha ndoto zao wanazozipigia huku akidai kuwa  mkoa wa Kagera unayofursa ya kutumia mashindano hayo kupata timu nzuri inayoweza  kupingana hadi kufika Ligi Kuu.

Saimoni Patick ambaye ni mwanasheria mkuu wa Yanga ametimiza haadi yake ya kuwa mdhamini mkuu wa mashindano haya ya Muhalila cup ambayo alitoa msimu wa tisa alipokuwa mgeni rasmi kwenye fainali za mashindano ambapo alihaidi kuongeza nguvu  ya kudhamini mashindano hayo.

“Mwaka Jana nilikuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo nilihaidi kuwa nitachukua vijana watakaoonyesha Vipaji vyao katika club mbalimbali na nitadhamini mashindano hayo kupitia taasisi yangu ya Wemfurebe Foundation ,nimefanya hivyo  na naamini Kwa furaha hii ya miaka 10  mashindano haya yataleta Vipaji vingi zaidi na vijana watafurahia kucheza soka,”alisema Patrick.

Ofisa Utamaduni Wilaya ya Muleba, Denis Joseph amesema mashindano hayo yamekuwa chachu ya kuibua vipaji kwa wachezaji  huku akisema kuwa ofisi  ya Mkurugenzi Wilaya ya Muleba kupitia Idara ya utamaduni  imekuwa ikihakikisha wachezaji wenye vipaji wanafikia malengo yao.

katika kuadhimisha mafanikio ya miaka 10 timu zinazoshiriki ligi hiyo zimepanda kutoka timu 16 hadi 18 huku mashindano hayo yakipongeza viwanja vya izigo na zimbihile ukilinganisha na kiwanja kimoja cha kagoma kilichokokuwa kinitumia ,mechi ya ufunguzi wa mashindano hayo ilizikutanisha timu  za Nsisha FC  na bukoba manispaa ambapo nsisha fc ilimfunga Bukoba Manispaa goli moja kwa sifuri 1_0

Fainali za mashindano hayo zitakuwa Desemba 31/2024.