Miliki bunifu kuwa chachu ya maendeleo
OFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa amesema WIPO imeendelea kuandaa mikakati na njia za kuhakikisha miliki ubunifu zinatumika kama chachu za maendeleo duniani.
Ameongea hayo jijini Dar es Salaam katika kikao cha mashauriano ya wadau kuhusu kujadili mkataba wa Sheria ya Kimataifa ya (WIPO) ya Ulinzi wa maumbo na michoro ya miliki ubunifu.
“Tanzania ni Moja ya nchi wanachama wa Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WiPO) na Shirika la Miliki Ubunifu la Kanda ya Afrika (ARIPO).
SOMA: BRELA itambue miliki bunifu -Mwana FA
“Kupitia mashirika haya nchi ya Tanzania, imesaini na kuridhia mikataba na itifaki mbalimbali zinazohusu usimamizi na uratibu wa miliki ubunifu kikanda na masuala mengine.
“Mikataba na hitifaki hizi zimewekwa mifumo Katika kuhakikisha usimamizi na uratibu thabiti wa miliki ubunifu Kimataifa ili kuendana na mabadiliko yanayoendelea duniani hasa Katika nyanja ya teknolojia na ubunifu.
Amesema kuwa WIPO zimeendelea kuandaa mikakati na njia za kuhakikisha miliki ubunifu zinatumika kama chachu za maendeleo duniani.
“Nchi wanachama wa WIPO zimeendelea kuandaa mikakati na njia za kuhakikisha miliki ubunifu inatumika kama chachu ya maendeleo Duniani hii imefanyika kwa kufanya majadiliano kwa kukabiliana kuanzisha Mikataba Katika maeneo muhimu ya umiliki ubunifu.
Amesema kuwa Kuna ushindani mkubwa wa biashara nje ya mipaka katika kuongeza ubora wa biashara na huduma.
” Kwa sasa Kuna ushindani mkubwa wa kibiashara nchini na nje ya mipaka ya nchi hasa Katika kuongeza ubora wa bishara au huduma na muonekano unaovutia wa bidhaa hivyo tunatakiwa kuhakikisha bidhaa zetu ikiwemo vifungashio na mikebe zinakuwa na ubunifu wa kipekee tunatakiwa kuhakikisha bidhaa au huduma ina muonekano unaovutia,” amesema Nyaisa.
Pia ameongeza kuwa watakwenda kufanya mafunzo kwa wanafunzi ili kuwajengea uwezo vijana wadogo ili mtoto awe na uelewa kuhusu ubunifu.
SOMA: Takukuru, Brela kushirikiana uchunguzi
Kwa upande wake Msajilii msaidizi kutoka ( BPRA) Mustafa Haki ambaye amumuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji BPRA Khamis Juma amesema kuwa sekta nzima inayohusina na miliki ubunifu Tanzania bara na Zanzibar inafanya kazi zake Katika kuhakikisha inashirikiana na mamlaka husika ili kuweza kupiga hatua gurudumu la maendeleo na uchumi kwa ujumla.
“Tumekuwa tukifanya kazi kwa pamoja Katika kutoa elimu,kushirikiana Katika Mikataba mbalimbali ya Kimataifa na Kitaifa kuhakikisha kwamba Tanzania inachukua kuona miliki ubunifu inafanikiwa kwa kiasi kikubwa,” amesema Haji.