Milioni 200 kwa watoto Muhimbili

DAR-ES-SALAAM : KIASI cha Sh milioni 200 kinatarajiwa kuchangwa kupitia mbio  za watoto(fun run) kupitia  programu ya Mtoto day out  itakayofanyika mwezi Disemba jijini Dar es Salaam.

Fedha hizo zitakazochangwa zitakwenda kusaidia watoto wenye changamoto za afya hasa wale wanaozaliwa utumbo ukiwa nje na wale wenyewe changamoto kwenye njia ya haja kubwa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mwanzilishi wa Programu ya Mtoto day out,Dina Marius amesema kwa miaka saba sasa wamekuwa wakifanya matukio yanayohusisha watoto kwa kupindi cha awamu mbili kwa mwaka mwezi Juni na Disemba na kukusanya watoto zaidi ya 3000 kutoka maeneno mbalimbali nchini.

“Kiliingilio huwa ni Sh 5000 kwa watoto ila sasa tumeona tusaidie watoto wengine tukifanya tunahusisha watoto yatima lakini kwa changamoto za kiafya tulikutana na Dk Zaituni  wa Muhimbili tukazungumza tatizo kubwa la mtoto anayezaliwa utumbo nje na gharama ni kubwa,”ameeleza.

Ameongeza “Tuko hapa kushirikiana na hospital ya Muhimbili na E fm kujenga uelewa kwa wazazi kuwa tatizo hilo linatibika na pia vifaa vya kurudisha utumbo ndani ni Sh 60,000 tunataka tukusanye wazazi wapate bure.

Amesema kwa mtoto ambaye amezaliwa na tatizo la njia ya  haja kubwa mpaka itengenezwe kuna kifaa kinauzwa Sh  25,000 vikiwa vinapatikana wazazi watapewa bure.

Dina amesema kwa watoto wanaozaliwa utumbo nje wanatamani kukusanya mifuko 2,000 na wenye tatizo la njia ya haja kubwa mifuko 2,000  ambapo  hilo litafanikishwa na  wadau na watanzania.

Amesema mchangiaji anatakiwa kuingia kwenye ukurasa wa      www.mtotodayout.tz.mtotodayout.tz na kuchangu ni wapi na kiasia  anachotakiwa  kuchanga ambapo mtoto mmoja atachanga Sh 35,000.

“Zawadi zitatolewa kwa watoto watakaoshinda mbio  na medali zitatolewa kwa watoto wote na zawadi zingine ,”Amesisitiza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Biashara wa E FM,Denis Busulwa amesema Mwaka huu mwezi wa saba walimlenga kuchangia kwa  mama na mtoto.

” Mwezi wa Julai,2024 tulifanya kampeni ya kutoa vifaa vya mama na mtoto tulikusanya 10,000 tulisambaza mkoa wa Dar es Salaam na Kisarawe, Pwani zilikuwa 5000 bado tunazo 5000 tutasambaza mikoa ya kusini.

Ameeleza kuwa sasa wameona ni vyema kuja na kampeni ya kusaidia watoto ambapo pia watatoa elimu kuhusu changamoto hiyo ili jamii iwe na uelewa mpana.

“Watu lazima wajue tatizo likoje na jinsi ya kuwasaidia watoto wenye tatizo na  E-fm  na Etv kwa kushirikiana na Muhimbili tutatoa elimu kwa miezi mitatu tutakuwa na mbio za watoto tutahamasisha jamii na wadau kuja kuchangia hii kampeni ili kukusanya fedha hizo na ni lengo ambalo litawezekana kwa kushirikiana.

Naye Daktari Bingwa Bobezi wa upasuaji kwa watoto wadogo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Zaituni Bokhary amesema awali aslimia 100 ya watoto waliokuwa wanazaliwa na tatizo hilo wanapoteza mai sha  lakini sasa wanaweza kuwasaidia watoto.

“Tunaendelea na utafiti ambao umeleta matokeo chanya kwa watoto hao sasa wanapatiwa huduma na kuishi kwani tunawapa huduma zinazotakiwa .

SOMA :Elimu Watoto njiti yaingizwa mtaala mpya wa elimu

Dk Bokhary amesema kwa wiki  kuna watoto watano hadi saba kwa wanaozaliwa njia ya haja kubwa na wanane kwa utumbo nje ambapo  namba inaongezeka hata 11 kwa wiki moja hivyo tatizo linaongezeka.

Habari Zifananazo

Back to top button