Mimi Mars arudi mazima kwenye filamu

MSANII wa Bongo Fleva, Marianne Mdee ‘Mimi Mars’ amesema kwa sasa anaweza kushiriki masuala yote ya sanaa baada ya kupata ruhusa kutoka kwa daktari wake kufuatia ukimya uliotokana na changamoto ya ajali ya gari.

Msanii huyo aliyetamba kwenye tathmilia ya Jua Kali alipata ajali Januari na kusababisha nafasi yake katika tamthilia hiyo kuchukulia na Elizabeth Michael ‘ Lulu’.

SOMA: Mimi Mars atamani mtoto

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mimi Mars amesema kuwa kwa sasa amerudi rasmi katika filamu.

“Kwa sasa nipo sawa na nimeruhusiwa na daktari wangu aliyekuwa akinipatia matibabu baada ya kupata ajali na nimerudi rasmi nitakuwa nikionekana katika tamthilia ya Jiya niliyocheza kama binti wa kimasai niliyesoma nje ya nchi.”

SOMA: Mimi Mars arejea kivingine

Kwa upande wake Rukhsaar Vazda maarufu kama ‘Jiya’ amemkaribisha Mimi Mars na kumpongeza kuwa ni msanii mwenye nidhamu.

Naye Breena Pinto (Jaya) ambaye anacheza kama mpenzi wa Mimi Mars kwenye tamthilia ya Njia amesema kuwa katika tamthilia hiyo wamekuwa wakishindana nani mkali.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Chugga Queen 🐝 (@mimi_mvrs11)

Habari Zifananazo

Back to top button