Miriam Odemba: Ulemavu sio mwisho wa ndoto

DAR ES SALAAM: ULEMAVU haumanishi kuwa unaweza kushindwa kutimiza ndoto zako msingi mkubwa ni kuwa na malengo, kazi na juhudi, anasema Mwanamitindo nguli Miriam Odemba.

Odemba amesema hayo leo Februari 19, 2026 wakati akizungumza kwa njia ya simu kutoka Ufaransa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam katika siku yake ya kuzaliwa.

Hafla hiyo imerudisha tabasamu jipya baada ya Taasisi ya Miriam Odemba Foundation inayomilikiwa na mwanamitindo huyo kuwapatia zawadi mbalimbali na kuwafturisha wanafunzi hao leo.

Odemba amewaambia watoto hao kuwa licha ya ulemavu walionao, ila bado wanaweza kuwa wanavyotaka.

“Watoto mnaweza kuwa madaktari, wasanii, viongozi, walimu, pia msituhusu hali yoyote mjione wadogo,” amesema Miriam Odemba.

Amewataka watoto hao kuendelea kusoma kwa bidii ili kutimiza malengo yao waliyojiwekea.

Kabla ya kupata futari, wanafunzi hao walipata nafasi ya kuonesha vipaji vyao mbalimbali ikiwemo kuimba, kucheza na ngoma za asili. Miriam Odemba alizaliwa Februari 19, 1982 jijini Arusha, ambapo leo amefikisha miaka 44 ya umri wake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Janeth Mteleke ametoa rai kwa wadau wa maendeleo kuona namna ya kugusa jamii ya wenye uhutaji hasa kipindi hiki cha kwaresma na mwezi wa Ramadhani.

SOMA ZAIDI:

Siku ya kuzaliwa: Odemba aungana watoto wenye uhitaji

“Nachoweza kusema wawakumbuke wenye uhitaji, una jirani anahitaji kampe, lakini pia tusiwe na israfu,” ameeleza Janeth.

Pia ameeleza namna wavyofurahia kugusa maisha ya watoto wenye uhitaji kwani kwa kufanya hivyo Mungu anawafungulia milango ya baraka zaidi.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I started this as a simple side hustle, and last month I made a little over $6,137 just working a few hours a day from my phone. If you want to check out how it works, the website has all the details.
    Here—>> http://www.giftpay7.vip

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button