Mjumbe CCM ataka ushirikiano uchaguzi serikali za mitaa

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa kupitia Jumuiya ya wazazi wa Chama Cha mapinduzi (CCM), Hamoud Abuu Jumaa, ameonya wanachama wa chama hicho kuacha tabia ya kuendeleza makundi na badala yake kushirikiana kwa pamoja katika kukipatia ushindi katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.

Akizungumza Katika ziara ya kikazi wilayani Kibaha vijijini mkoani Pwani, Hamoud, alisema katika kipindi hiki ambacho chama hicho kinajiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka 2024, makundi hayahitajiki.

Alisema wajibu wa wanachama na viongozi ni kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo na kwamba jambo hilo litawezekana iwapo watachukua hatua ya kuthibiti makundi na kuyavunja kwa maslahi ya (CCM)

“Makundi hayahitajiki lengo letu ni moja kushinda. .niwaombe ndugu zangu wakati tunajiandaa kwenda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa tuvunje makundi na kuacha kuyaendeleza”alisema

“Tufanyekazi kuhakikisha Chama chetu kinaendelea kushinda…kwa sasa nasikia kuna mambo ya uchawa suala la uchawa sio sera ya CCM na hilo halipo Ila hamkatazwi kuwa na makundi ya aina hiyo ili mradi lengo liwe lenye maslahi ya chama”alisema.

Aidha aliitaka Jumuiya ya wazazi kuendelea kubuni vya bora vya mapato hatua ambayo itaisaidia Jumuiya hiyo kuinuka kiuchumi.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Pwani, Jackson Kituka, aliwataka wanachama hao kuunga mkoni jitihada za serikali na Chama ikiwa ni pamoja na kusimamia vema miradi ya maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Morogoro, Rose Rwakatare aliliwataka waancha wa jumuiya hiyo kujilita katika katika misingi ya maadili ikiwa ni pamoja na kuwa mstari wa mbele kukemea vitendo vyote vya ukiukwaji wa maajili.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
neknoyirze
neknoyirze
3 months ago

Earn income while simply working online. work from home whenever you want. just for maximum 5 hours a day you can make more than $600 per day online. From this I made $18,000 last month in my spare time.

Check info here==============>>>   http://www.join.hiring9.com

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x