Mkurugenzi INEC apiga kura Dodoma
MKURUGENZI wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Kailima Ramadhani amejitokeza kupiga kura kwenye Kituo cha Shule ya Msingi Chaduru, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, mkoani Dodoma.
Baada ya kupiga kura amekagua vituo vya kupiga kura vya Shule ya Msingi Kisasa, Chaduru na Kituo cha Chilewa kilichopo katika Ofisi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Chilewa, Chang’ombe, jijini Dodoma.
SOMA: Uchaguzi Mkuu Oktoba 29
Watanzanzia kote nchini leo wanapiga kura kwenye Uchaguzi wa Rais, Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara.
Uchaguzi huo unafanyika chini ya kauli mbiu “Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura” ambapo vituo vimefunguliwa saa 1:00 asubuhi na vitafungwa saa 10:00 jioni.



