Mkurugenzi PURA aeleza nafasi ya teknolojia sekta ya petroli

DAR ES SALAAM: Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mhandisi Charles Sangweni amesema ukuaji wa teknolojia una mchango mkubwa katika maendeleo  ya sekta nzima ya petroli.

Mhandisi Sangweni ameyasema hayo Mei 27, 2025 wakati akifungua Mkutano wa Teknolojia Afrika jijiji Dar es Salaam.

Mkutano huo ulioandaliwa na Jumuiya ya Wahandisi wa Petroli nchini kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wahandisi wa Petroli Kanda ya Afrika umewaleta pamoja washiriki takriban 200 kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kujadili maendeleo ya tasnia ya petroli na kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali.

SOMA: SONGOSONGO| Wajumbe PURA wakunwa na miradi ya CSR

Miongoni mwa maeneo hayo ni pamoja na teknolojia za kisasa zinazotumika katika shughuli zinazotekelezwa katika mnyororo wa thamani wa petroli kama vile kuzalisha, kuchakata na kusafirisha Rasilimali za petroli.

Akitilia mkazo matumizi ya teknolojia, Sangweni alieleza umuhimu wa kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi na uzoefu wa matumizi ya teknolojia za kisasa zinazotumika katika tasnia hii.

Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Teknolojia Afrika unaofanyika jijini Dar es Salaam Mei 27 hadi 29, 2025.

“Ni muhimu kuwaandaa vijana wetu na wataalamu wetu kuendana na teknolojia au mabadiliko ya teknolojia yanayoendelea duniani” alisisitiza Sangweni.

Sangweni pia aligusia suala la matumizi ya akili mnemba katika kutekeleza majukumu wanayofanya wahandisi wa petroli na kuwataka wanajumuia hiyo kuendelea kujiongezea maarifa katika eneo hilo muhimu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button