Mkutano wa 62 wa Bodi ya EITI waing’arisha Tanzania

Katika hatua ya kihistoria kwa sekta ya uchimbaji wa madini,Tanzania imekuwa mwenyeji wa  mkutano wa 62 wa bodi ya kimataifa ya uwazi na uwajibikaji, (Global Extractive Industries Transparency Initiative – EITI)  uliofanyika hivi karubuni

Mkutoano huo muhimu uliyofanyika jijini Arusha, umekuwa ni uthibitisho wa hatua kubwa ambayo Tanzania imepiga  kimataifa katika uwazi, uwajibikaji, na taratibu endelevu za uchimbaji wa madini. Mkutano huo uliwaleta pamoja wahusika muhimu kutoka serikalini, asasi za kiraia, na sekta binafsi kujadili masuala muhimu yanayokabili sekta ya uchimbaji na kuimarisha umuhimu wa usimamizi wenye uwajibikaji wa rasilimali.

Fursa ya kuwa mwenyeji wa  mkutano  huo wa bodi ya EITI ilipatikana baada ya majadiliano ya kiwango cha juu yaliyoongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa New Zealand na mtetezi mashuhuri wa maendeleo endelevu, Helen Clark, mnamo Aprili 2024, alipoitembelea Tanzania.

Advertisement

Kuchaguliwa kwa  Tanzania kama nchi mwenyeji kulionyesha msimamo thabiti wa Tanzania kwa uwazi na uwajibikaji katika sekta ya uchimbaji wa madini na zaidi sana umekuwa kielelezo cha kutambulika na kuthaminiwa kwa juhudi za Tanzania katika kutengeneza rafiki kwa uwekezaji ambayo yana usawa wa ukuaji wa kiuchumi na uwajibikaji wa kijamii na kimazingira.

Sekta ya uchimbaji Tanzania, ambayo inajumuisha madini, mafuta, na gesi, kwa muda mrefu imekuwa kiungo muhimu cha uchumi wake. Kwa kukaribisha Mkutano wa Bodi ya EITI, Tanzania ilionyesha juhudi zake za kufuata uzoefu bora wa kimataifa na kuimarisha imani kati ya wawekezaji wa kimataifa.

Mkutano huo ulikuwa jukwaa la kuonyesha maendeleo ya Tanzania katika utekelezaji wa moja ya kigezo cha EITI, ambacho kinakuza usimamizi wa wazi na wenye uwajibikaji wa rasilimali asilia.Kama mshiriki muhimu namdhamini mkuu wa hafla hiyo, AngloGold Ashanti Tanzania ilichukua jukumu muhimu katika kuweka Tanzania kama kivutio cha juu cha uwekezaji wenye uwajibikaji katika sekta ya uchimbaji.

Juhudi za kampuni hiyo za uzoefu endelevu wa uchimbaji wa madini na kuwezesha jamii, zilikuwa mada kuu katika majadiliano yote.

Akizungumza katika hafla hiyo, Simon Shayo, Makamu wa Rais – Uendelevu na Maswala ya Biashara (Afrika) wa AngloGold Ashanti, alisisitiza dhamira ya kampuni hiyo katika kutekeleza wajibu wake.

“Kauli yetu ni rahisi: tunachimba madini ili kuwezesha watu na kuendeleza jamii. Kila tunachofanya kinaendana na dhamira hii, na majadiliano ya leo yanathibitisha kwamba katika uchimbaji wa madini, kila mtu ana jukumu la kufanya,” alisema Shayo huku washiriki wakionyesha umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, kampuni, na jamii  ili kuhakikisha kwamba uchimbaji wa madini unakuwa na faida wahusika wote.

AngloGold Ashanti Tanzania imekuwa muongoza njia katika kukuza uwazi na uendelevu katika sekta ya madini.Miradi ya kampuni hiyo inajumuisha uwekezaji katika jamii za wenyeji, kusaidia mipango ya elimu na afya, na kufanya uchimbaji wa madini wenye uwajibikaji wa kimazingira.

Kwa kufuata kanuni za EITI, AngloGold Ashanti Tanzania imekuwa kipimo cha rejea kwa kampuni zingine katika sekta hiyo.

 

SOMA: Ushirikiano Tanzania, Korea kuleta mageuzi sekta ya madini nchini

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *