Ushirikiano Tanzania, Korea kuleta mageuzi sekta ya madini nchini

Naibu Waziri wa Madini Dk Steven Kiruswa.
NAIBU Waziri wa Madini Dk Steven Kiruswa amesema kutokana na kuongezeka kwa mahitaji na matumizi ya Madini Muhimu duniani, Tanzania ina dhamira ya dhati ya kuendeleza Sekta ya Madini ikiwa ni pamoja na Madini Mkakati hapa nchini kwa kuimarisha ushirikiano na Korea Kusini kwa lengo la kuleta mageuzi yenye kuleta tija zaidi kupitia sekta hiyo.
Ameyasema hayo leo Machi 25 jijini Seoul, Korea Kusini wakati akizungumza katika Mkutano wa Madini Muhimu kati ya Tanzania na Korea ulioandaliwa jijini humo.
Dk Kiruswa amesema kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA) ya mwaka 2023, matumizi ya lithiamu yameongezeka kwa asilimia 30, huku mahitaji ya nikeli, kobalti, kinyewe (graphite), na madini adimu yakiongezeka kati ya asilimia 8 hadi 15 na kwamba hali hiyo inatoa fursa kubwa kwa Tanzania kushirikiana na mataifa yenye teknolojia za kisasa kama Korea katika uchimbaji, uongezaji thamani, na biashara ya madini haya.
Aidha, Dk Kiruswa amesisitiza kuwa, Tanzania ni nchi yenye utajiri mkubwa wa madini yanayohitajika kwa teknolojia za kisasa, hususan nishati mbadala.
“Tanzania ina hifadhi kubwa ya madini kama vile grafiti, nikeli, kobolti, lithiamu, madini adimu (REE), shaba, manganese, zinc, dhahabu, na vito vya thamani, ambavyo vinahitajika kwa maendeleo ya viwanda vya teknolojia na nishati safi,” amesema Dk Kiruswa.
Sambamba na hilo , Dk Kiruswa amebainisha kuwa, katika jitihada za kuhakikisha sekta ya madini inawanufaisha Watanzania, Tanzania inalenga kuongeza thamani ya madini yake ndani ya nchi kabla ya kuuza nje.
“Tunatambua uwezo mkubwa wa Korea katika teknolojia za uchimbaji, utafiti, na uchenjuaji wa madini. Ushirikiano wetu utaleta manufaa kwa pande zote mbili,” ameongeza Naibu Waziri.
Katika hatua nyingine, Dk Kiruswa amepongeza Kampuni za Kikorea kama POSCO International, inayoshiriki katika mradi wa Mahenge Graphite, na Yulho, ambayo imewekeza katika uchimbaji wa nikeli kusini mwa Tanzania na kwamba uwepo wa Kampuni hizo hapa nchini ni ushahidi kwamba Tanzania ni mahali salama.
3 comments
  1. ᴇᴀʀɴ 𝟣𝟪𝟢𝟢+ ʙᴜᴄᴋꜱ ᴡᴇᴇᴋʟʏ ꜰʀᴏᴍ ʜᴏᴍᴇ! ᴀ ꜰᴇᴡ ᴍᴏɴᴛʜꜱ ᴀɢᴏ, ɪ ᴡᴀꜱ ꜱᴛᴜᴄᴋ ɪɴ ᴀ ʀᴏᴜᴛɪɴᴇ, ʙᴀʀᴇʟʏ ᴍᴀᴋɪɴɢ ᴇɴᴅꜱ ᴍᴇᴇᴛ. ɴᴏᴡ, ɪ ᴇᴀʀɴ 𝟤𝟢𝟧+ ᴀ ᴅᴀʏ ᴡᴏʀᴋɪɴɢ ꜰʀᴏᴍ ʜᴏᴍᴇ ᴡɪᴛʜ ᴄᴏᴍᴘʟᴇᴛᴇ ꜰʟᴇxɪʙɪʟɪᴛʏ! ɴᴏ ᴇxᴘᴇʀɪᴇɴᴄᴇ? ɴᴏ ᴘʀᴏʙʟᴇᴍ. ᴛʜɪꜱ ɪꜱ ᴀ ʀᴇᴀʟ ᴏᴘᴘᴏʀᴛᴜɴɪᴛʏ ᴛᴏ ʙᴜɪʟᴅ ꜰɪɴᴀɴᴄɪᴀʟ ꜰʀᴇᴇᴅᴏᴍ ᴏɴ ʏᴏᴜʀ ᴛᴇʀᴍꜱ.

    ᴊᴏɪɴ ɴᴏᴡ➤➤ http://Www.WorksProfit7.Com

  2. Thank yoou a lot for sharing this wirh all of uus
    yyou actuaally recognize wjat you’re talking approximately!
    Bookmarked. Kindlly also conslt with my sote =). We mayy
    hve a link alternate agreement amng us

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *