Mndeme alipania jimbo la Kigamboni, atwaa fomu ubunge

DAR ES SALAAM: DHAMIRA, maono na uthubutu unaendela kutawala hisia za Wakili Mwanaisha Mndeme ambapo leo Aprili 30 amechukua fomu kuomba ridhaa ya kugombea ubunge Jimbo la Kigamboni kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.

Akizungumza leo na waandishi wa habari, mara baada ya kuchukua hiyo, Mwanaisha amesema endapo akipata ridhaa ya kuwa Mbunge wa Kigamboni atatua changamoto zinazowakumba wananchi wake na kufanya kuwa sauti ya Kigamboni.

Eneo kubwa ambalo Mwanaisha anatazamia kulifanyia kazi endapo akichaguliwa ni miundombinu ambapo amesema kwa muda mrefu wananchi wa eneo hilo wamekuwa na changamoto hiyo.

“Leo hii kigamboni kuna changamoto kubwa ya miundombinu kwa mfano kata ya PembaMnazi,Kata ya Kisarwe 2 hakuna kabisa Barabara, wananchi wanalazimika kutumia hela nyingi kusafiri, nikipata nafasi ya Ubunge nitahakikisha naziondoa hizi changamoto,” amesema Mwanaisha.

Amesema pindi akipata Ridhaa ya Mbunge wa kigamboni atapigani sera ya uhifadhi kwa wavuvi ili waweza kunufaika na mifuko ya uhifadhi ya jamii ikiwemo kupata mafao .

“Nitakuwa sauti ya wavuvi maana kigamboni watu wengi ni wavuvi ili kutatua changamoto zinazowakumba wavuvi ili wavuvi waweze kufanya kazi zao bila kikwazo,” amesema Mwanaisha.

Kuhusu sera na sheria, Wakili Mwanaisha amesema pindi akipata ridhaa ya kuwa mbunge wa Kigamboni atatumia taaluma yake ya sheria kuhakikisha zinatungwa sheria zitakazoweza kulinda maslahi mapana ya rasilimari za nchi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button