Mo awapongeza Yanga

“Hongera sana mtani, umeifanya umeifaharisha Tanzania. Karibu kwenye michuano mikubwa.” Ameandika Rais wa heshima wa Simba SC, Mohammed Dewji ‘Mo’ amesema siku moja baada ya Yanga kufuzu hatua ya makundi kwa kumtandika Club Africain bao 1-0 nchini Tunisia.

Baada ya ushindi huo, Yanga sasa inasubiri droo ya hatua ya makundi itakayofanyika Jumatano ya Novemba 16 Cairo Misri, kuona itapangiwa na timu zipi katika hatua hiyo.


Mismu wa 2015/2016 Yanga ilifuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo na kupangiwa na timu za TP Mazembe, Mo Bejaia na Medeama na Yanga kumaliza nafasi ya mwisho ikiwa na pointi nne kwenye msimamo wa kundi A.

Msimu wa 2018 Yanga iliingia tena katika makundi na kupangiwa na timu za USM Ulger, Rayon Sports na Gor Mahi na Yanga kumaliza nafasi ya nne ikiwa na pointi nne katika msimamo wa kundi D.

Timu zingine zilizofuzu hatua ya makundi ni Asec Mimosas, ( Ivory Cost) TP, Mazembe, (DRC Congo), Pyramids, ( Misri) Monastir, ( Tunisia) FAR Rabat, ( Morocco) Rivers United, ( Nigeria) Motema Pembe (DRC Congo), Plateau United ( Nigeria) na nyinginezo.

Kwa upande wa timu zilizofuzu makundi Ligi ya Mabingwa ni Al Ahly (Egypt), Al Hilal (Sudan), Al Merrikh SC (Sudan), Atletico Petroleos (Angola), Coton Sport (Cameroon), CR Belouizdad (Algeria) Esperance Tunis (Tunisia), Horoya (Guinea), JS Kabylie (Algeria), Mamelodi Sundowns (South Africa), Raja CA (Morocco), Simba SC (Tanzania), Vipers SC (Uganda), Wydad AC (Morocco), Zamalek (Egypt), AS Vita Club (RD Congo).

Habari Zifananazo

Back to top button