Mo yupo sana -Try Again

MASHABIKI wa Simba wamepewa taarifa njema kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try again’ kuwa mwekezaji Mohammed Dewji yupo sana Msimbazi.

Hatua hiyo huenda ikawa ni baada ya jana Mo Dewji kuandika kupitia Twitter yake kuwa kuna ambao wanakwamisha mchakato wa uwekezaji hali inayomfanya aanze kukata tamaa.

Tweet ya Mo ambayo baada ya muda aliifuta ilisomeka “Transformation ya Simba bado haijakamilika huu ni mwaka wa 6.

Karibuni ntakata tama.” Aliandika Mo.

Akizungumza leo Juni 12, 2023 kwenye tukio la Unyama Mwingi linaloendelea viwanja vya Leaders Club, Salim Abdallah amesema: “Mohammed Dewji bado yupo sana Simba na ataendelea kuwepo.”

Habari Zifananazo

Back to top button