Huduma za kibingwa zafika kanda ya kati

DAR ES SALAAM: TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imepeleka huduma za kibingwa na bobezi kwa wananchi walioko mikoa ya kanda ya kati ikiwemo Dodoma.
Huduma zimeanza kutolewa jana katika kwanza cha Chinangali Park, Dodoma ambapo Daktari Bingwa Mbobezi wa mifupa MOI, Dk Tumaini Minja ameeleza huduma ambazo wananchi wanazipata katika banda la MOI.
“Katika wiki hii ya utumishi wa umma tunatoa huduma ya ushauri wa kibingwa na bobezi za Mifupa, Ubongo, Mgongo, Mishipa ya fahamu pamoja na utengamao” amesema Dk Minja.
Ameongeza ” Jopo la Madaktari na Watalaam tupo hapa kwa ajili ya kuhudumia wananchi ikiwa ni sehemu ya utumishi bora.
SOMA ZAIDI
Naye Sharif Masoud, mkazi wa Bukoba amefurahishwa na huduma bora aliyoipata alipotembelea banda la MOI.
“Nilikuwa na shida ya mgongo kwa mda kidogo na nashukuru Madaktari na Wataalam kutoka MOI wapo hapa wamenipa huduma bora ambayo ntaifanyia kazi ili kuweza kuondokana na maumivu ya mgono” amesema Sharif.
Wiki ya utumishi wa umma imeanza Juni 16, 2025 na iafikia tamati Juni 23, 2025 na Taasisi ya MOI itatoa huduma hizo bure wakati wa wiki hiyo.