Morocco imeweka rekodi kwa mara ya kwanza ya kuwa timu pekee kutoka Afrika kuingia hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Ureno bao 1-0. Bao la pekee limefungwa na Yusuf En Nesyri dakika ya 42.
Tangu kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1930 Morocco inakuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kuingia nusu fainali ya mashindano hayo. Timu hiyo sasa itakutana na mshindi wa England na Ufaransa.
Mwaka 1989 Morocco iliondolewa 16 bora na Ujerumani kwa kufungwa bao 1-0, lakini ilifika hatua hiyo, badaa ya mchezo wao wa mwisho wa makundi kuifunga Ureno mabao 3-1.
Walau ilikuwa Cameroon aliyekuwa anakaribia nusu fainali mwaka 1998, ambapo aliondolewa kwenye robo na England kwa kufungwa mabao 3-2. Mwaka 2002 Senegal nayo ikaondolewa na Uturuki kwa kufungwa bao 1-0.
Mwaka 2010 nchini Afrika kusini, Ghana ikaondolewa na Uruguay na kuua ndoto za timu za Afrika kucheza nusu fainali.