Watu watatu wamekufa ajali ya moto

WATU watatu wa familia moja wamekufa na mmoja kunusurika baada ya ajali ya moto iliyotokea katika moja ya nyumba zilizopo katika Mtaa wa National, Kata ya Magu, Halmashauri ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

Waliokufa ni Mwakibeta Mathew (62) anayedaiwa kuwa mke wa manusura aliyejulikana kama Mzee Mtagala pamoja na dada Luberata Ngwata (40) na mjukuu Neema Kizinga (18) ambaye alikuwa anasoma kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Magu.

Akizungumza katika eneo la tukio jana, Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Magu, Mkaguzi wa Polisi, Gaston Tibulebwa amesema  jeshi hilo linaendelea kuchunguza chanzo cha ajili hiyo ya moto huku akitoa mwito kwa wananchi kuwa makini kwa matumizi ya vifaa vya umeme.

Pia, Tibulebwa amewataka wananchi kuwa wepesi kutoa taarifa kwa wakati pale changamoto inayojitokeza kwa kila mmoja kuwa makini na kuona ni wajibu wake kila anapoliona jambo na kulitolea taarifa. SOMA: Watu 63 wafa ajali ya moto Afrika Kusini

Nae Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jubilate Lawuo amesema ili kuweza kuzuia na kukabiliana na majanga ya moto ni vyema kila mtu kuwa makini juu ya matumizi ya teknolojia ya umeme ili kuweza kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

Moto huo unasemekana ulianza kuwaka majira ya saa 6 usiku lakini watu waliuona saa 7 usiku ndipo walipoanza jitihada za kuuzima. Ilielezwa kuwa miili ya wote waliokufa imehifadhiwa, wakati manusura akiendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa Bugando.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button