Mradi upanuzi wa maji wafikia 92% Bukoba

WANANCHI zaidi ya 18000 wa kata sita za Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera waliokuwa na changamoto ya maji kwa muda mrefu wanatarajia kunufaika na mradi wa maji safi na salama utakaogharimu Sh bilioni 3 hadi kukamilika.

Akisoma taarifa ya mradi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA) Mhandisi Daudi Beyanga amesema kuwa mradi huo katika utekelezaji wake umefikia asilimia 92.

Advertisement

SOMA: Mwenge wa Uhuru kukagua miradi ya Sh bilioni 1 Ukerewe

Baadhi ya wananchi wa kata hizo akiwemo Denice Kalugendo na Plasidia Alkadi wamesema kuwa mradi huo unaenda kutatua changamoto ya maji kwani wamekuwa wakifata maji umbali mrefu ambayo pia huchafuliwa na mifugo.

SOMA: Mwenge wa Uhuru wakagua miradi ya Sh Bil 5 Iramba

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Godfrey Mnzava wakati akitembelea mradi huo amesema kuwa utekelezaji unaendelea na ukikamilika utasaidia wananchi kupata huduma ya maji safi na salama.

Ujenzi wa mradi huo wa upanuzi wa mtandao wa maji kwa Manispaa ya Bukoba unaotekelezwa kwa awamu mbili, ulianza kutekelezwa Desemba 2020 na unatarajia kukamilika Desemba 2024.