Mradi wa maji Geita kufanyiwa majaribio 2025
MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita (GEUWASA) imeeleza ifikapo Juni 2025 mradi wa maji wa miji 28 wilayani Geita utafanyiwa majaribio kabla ya kukabidhiwa rasmi Desemba 2025.
Mradi huo wilayani Geita unatekelezwa kwa gharama ya Sh bilioni 124 ukihusisha ujenzi wa matenki matano ya maji, kituo cha kupokea maji, kituo cha kutibu maji na usambazaji wa mabomba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Geuwasa, Mhandisi Frank Changawa amesema hayo wakati akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Maji Geuwasa mara baada ya kukagua mradi huo ulioanza kutekelezwa Aprili 2024.
“Tunaenda kujenga intake ya lita milioni 46, tupo na mtambo wa kutibu wa lita milioni 45, harafu tutakuwa na bomba la kusafirisha maji kwa zaidi ya kilomita 50,” amesema Mhandisi Changawa.
SOMA: Geita kuongeza weledi usimamizi miradi ya maji
Amesema mpaka sasa matenki matatu kati ya matano ya kupokea na kusambaza maji yameshakamilika huku matenki mawili makubwa ujenzi wake unaendelea ambapo pia ujenzi wa eneo la chanzo umeanza tayari.
“Huu ni mradi mkubwa ambao utaenda kuleta lita milioni 45 kwa siku kwa mji wa Geita kwa wakazi wote wa kata 13, pamoja na vijiji 19 vitakavyopitiwa na bomba kubwa la maji kutoka ziwani.
“Kwa sasa mahitaji ya maji mjini Geita ni lita milioni 22 kwa wastani lakini tutaweza kuzalisha lita milioni 45 kwa hiyo tutakuwa na uwezo wa kuzalisha mara mbili ya hiki ambacho tunazalisha sasa hivi,” amesema Changawa.
SOMA: Geita wavunja mkataba na mkandarasi wa maji
Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Geuwasa, Patricia Kampambe amekiri kuridhishwa na mwenendo wa kazi na kueleza kuwa ana imani mradi utakamilika kabla ya Desemba 2025 kama ilivyopangwa.
“Tunaona jinsi ambavyo kazi inafanyika, imefanyika katika ubora, imefanyika vizuri na tunaamini kabisa kwamba utendaji ni mzuri,” amesema Patricia.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Geuwasa, Mhandisi Paul Chama amewaomba wakandarasi kuongeza kasi na kutekeleza mradi kulingana na usanifu wa wizara ili malengo yafikiwe kwa wakati.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu( Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi ametembelea Mradi wa Maji Mshikamano uliopo Kata ya Mbezi, Wilaya ya Ubungo katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Ubungo ambapo amemshukuru na kumpongeza Mhe. Raisi Samia… pic.twitter.com/OyLHxshwvB
— DAWASA (@dawasatz) September 19, 2024