Mradi wa mil 710/- kufungua fursa zao la mkonge

TANGA: Ujenzi wa kiwanda cha kisasa cha kuchakata mkonge kilichogharimu Sh milioni 710 katika kijiji cha Taula Wilaya ya Handeni mkoani Tanga unatarajiwa kuibua fursa mbalimbali kwa wakulima ikiwemo ajira na kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Profesa Esther Dungumaro wakati bodi hiyo ilipotembelea miradi ikiwamo Shamba la Mkonge Kibaranga ambalo linafanyiwa ukarabati wa miundombinu ya uchakataji mkonge na mradi wa ufugaji, mruazi.

Prof. Dungumaro amesema maboresho kama hayo yanaendelea katika sehemu mbalimbali yakianzia mkoani Tanga.

Kilimo cha Mkonge kina fursa – Maghali

“Handeni ni eneo mojawqpo ambalo tunajenga kiwanda cha kuchakata Mkonge. Ikumbukwe Serikali ya Awamu ya Sita imehamasisha sana wakulima wa zao la Mkonge miaka mingi iliyopita zao hili lilikuwa linaibeba nchi yetu kitaifa na kimataifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti Cha,ma cha Ushirika cha Kibaranga (Kibaranga Amcos), Paulo Haule amesema kwa ukarabati unaoendelea licha ya ajira lakini utawaingizia kipato kwani wakulima wa Muheza na majirani zetu ambao ni Wilaya ya Mkinga watapata fursa ya kupeleka Mkonge wao badala ya kupeleka maeneo mengine.

“Tunamshukuru Rais kwa kutuwezesha sisi wakulima wadogo kupata viwanda kama hivi na kukarabati kiwanda chetu ili hatimaye wananchi waweze kuboresha maisha yao,” amesema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button