Msalala waanza kutoa mikopo vijana, wanawake

HALMASHAURI ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeanza mipango ya kutoa mikopo asilimia 10 kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye walemavu.

Ambapo zaidi ya Sh Bilioni 1.8 zimetengwa kutoka kwenye mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita mara baada ya kufunga mafunzo ya utumiaji wa mfumo mpya wa usajili vikundi kwa njia ya kielekloniki kwa maofisa maendeleo ya jamii kutoka kata 18.

Advertisement

Mhita amesema ofisa maendeleo ndiyo wasimamizi wakuu wa fedha hizo wamepewa mafunzo ili kuimarisha vikundi na kusiwepo kikundi hewa kama ilivyokuwa miaka iliyopita.

SOMA: Mikopo 10% yaiva, mfumo, kanuni tayari

“Kamati za ufuatiliaji zimeundwa tayari zitakuwepo kwenye ngazi za kata na wilaya kuhakikisha vikundi vinafutiliwa kwa umakini lengo fedha zitumike kukopwa na kurudishwa kama ilivyolengwa kwenye makundi hayo,”amesema Mhita..

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Mary Nziku ambaye ni ofisa utumishi amesema fedha hizo zinatolewa katika makundi ya wanawake asilimia 40, vijana asilimia 40 na watu wenye ulemavu asilimia 20.

“Kwa kikundi cha wanawake wametengewa Sh milioni 434, kikundi cha vijana Sh milioni 434 na kikundi cha watu wenye Ulemavu Sh milioni 217,”amesema Nzuki.

SOMA: Watakiwa kujiunga vikundi fursa za mikopo

Ana Mwakalinga ofisa maendeleo ya jamii kutoka kata ya Bugarama amesema utaratibu wa kujisajili kupitia mfumo imani iliyopo kutakuwa na uangalizi mkubwa kwa watu wengi tofauti na zamani ilikuwa kwa maafisa maendeleo pekee.

Ofisa Maendeleo ya jamii kata ya Mwaluguru Julius Sungura amesema kwa mujibu wa kanuni mpya zilizotolewa juu ya vikundi kupata asilimia kumi wanaweza kujisajili wenyewe kwenye mfumo na hakutakuwepo mikopo yenye ujanja ujanja nakutimiza adhima ya Rais kwa makundi yote kunufaika.