MSD, wadau wajadili kuimarisha huduma za Afya Kagera

Wakurugenzi kwa kushirikiana na waganga wakuu wa wilaya mkoani Kagera wametakiwa kutumia vyanzo vingine vya mapato kulipia madeni yote ya dawa walizoziagiza Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kurahisisha upatikanaji dawa katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasito Siima ametamka hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatuma Mwassa katika mkutano mkuu wa wateja na wadau wa MSD Kanda ya Kagera ambao hufanyika kila mwaka.
“Baadhi ya zahanati, vituo vya afya na hospitali zimelipa vizuri madeni yao lakini baadhi bado hawajalipa madeni, hii inaweza kuathiri mfumo wa utoaji huduma katika maeneo yetu,”anasema Siima.
Amekiri kupokea deni la shs Bilioni 6.3 la Halmashauri 11 zinazohudumiwa na Bohari hiyo, hivyo akatoa wito kwa wakurugenzi kuhakikisha wanalipa haraka ili huduma ziendelee kuwa nzuri katika vituo vya Afya.
Katika mkutano huo vyeti vya kutambua wateja bora, Halmashauri na hospitali zilizofanya vizuri kwa kuagiza dawa kwa wakati na kupunguza madeni kwa mwaka 2023/2024 vimetolewa.

Habari Zifananazo

Back to top button